Wednesday, 14 January 2015

Watanzania wanyongwa kwa mihadarati

 NA EMANUEL MASAO

 


 Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania.


Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye kwa sasa anafanya ziara maalum Tanzania, amesema yeye ndiye ambaye amekuwa akisambaza barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa wanaoshikiliwa kwenye magereza hayo ambapo baadhi yao wametaja majina ya watu wanaodaiwa kuwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliowatuma kusafirisha dawa hizo.

Padre Wotherspoon amefika kuonana na familia za wafungwa hao pamoja na idara za serikali zinazohusika na mapambano dhidi ya biashara hiyo hatari ya dawa za kulevya. Mwandishi wetu Ben Mwang'onda anasimulia zaidi kutoka Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment