Na dulla wellah , ruaha media
15th January 2015
B-pepe
Chapa
Idadi hiyo imeongezeka katika mkoa wa kipolisi Temeke ambapo kwenye operesheni ya juzi wahalifu hao walikamatwa 47 na kuongeza idadi ya kufikia 1,4 38.
Aidha vijana hao walikamatwa ni pamoja na wapiga debe katika vituo vya daladala, wacheza kamari, wavuta bangi, watumiaji wa dawa za kulevya na watumiaji wa gongo.
Akizungumza na waandishi wa habari j, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke, Kihenya Kihenya, alisema juzi waliwakamata vijana 47 ambapo idadi Kamili inafikia 289.
Hata hivyo NIPASHE iliwatafuta Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, Mary Nzuki, simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa na Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura, alituma ujumbe wa meseji uliosema yupo kwenye kikao.
Joyce Mbaruku, mkazi wa Magomeni akizungumza na NIPASHE, alisema operesheni hiyo inayofanywa na Jeshi la Polisi ni ya uonevu kwani wanakamata watu hovyo bila ya kufanya uchunguzi na kuwahusisha na kundi la ‘Panya road’.
Alisema ameshangazwa na taarifa za kukamatwa kwa vijana wake wawili huku wakihusisha na kundi hilo kwani tabia za watoto wake anazijua vizuri na katika mtaa huo walipokamatiwa ni wageni na hawajawafahamu vizuri wenyeji wa mtaa huo.
“Taarifa hizi za kukamatwa kwa watoto wangu nimezipata kwa masikitiko makubwa sana kwani vijana wangu katika mtaa huu ni wageni ni juzi tu tumeamia kutoka Shekilango hivyo Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya upelelezi kwanza ili kuwabaini watu wanaowatafuta na kuwakamata,” alisema.
Filibert Mboya, mkazi wa Mwenge, ameshangazwa na operesheni hiyo kwa kusema vijana wengi waliokamatwa hasa katika maeneo ya Mwenge hawahusiki na kundi hilo la uhalifu.
Alisema rafiki zake watatu pamoja na mtoto wa kaka yake walikamatwa katika uwanja wa mpira Mwenge wakiangalia mazoezi ya mpira wa miguu ndipo Polisi walipotokea na kuanza kuwakamata.
“Watu waliokuwepo uwanjani baada ya kuona polisi walikimbia sana kwani walipiga risasi za moto mbili juu na nyingine za mabomu hivyo wapita njia na watu waliokuwapo uwanjani hapo walishikwa na butwaa na kuanza kukimbia kila kona hivyo ndugu zangu hao wakakamatwa kutokana na kuzidiwa na moshi wa bomu la machozi,” alisema Mboya.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo, alisema siyo ya kweli kwani operesheni hiyo inaendeshwa kwa kufuata taratibu zote na taarifa za vijana wanaokamatwa zinatoka kwa wazazi wao.
Aliongeza kuwa kama kuna watakaobainika kutohusika tawaachiwa huru.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment