Wednesday, 14 January 2015

MCHEZAJI ADHALILISHWA KIJINSIA

 na esther danford, ruaha media


 
Genoveva Anonma
Genoveva Anonma alidhalilishwa,kwa takriban miaka minne,amekuwa akihisiwa kuwa si mwanamke naye amekuwa akizidharau tuhuma hizo mara kwa mara.
Lakini kuna kitu ambacho hakukitegemea kilichokuwa kinamuandama kufuatia uwezo wake michezoni alipokuwa Equatorial Guinea mwaka 2008 katika michuano ya soka la wanawake wa mataifa ya Afrika.
Goli lake la ushindi katika ardhi ya nyumbani,na timu yake kuwa ya kwanza wakiifuatia Nigeria ,ambayo iliibuka kuwa washindi wa jumla,Anonma badala ya kuhesabika kuwa mkombozi na mwenye kuitimiza ndoto yake michezoni, badala yake amebaki njia panda.
Anonma awapo uwanjani huwa ana haha uwanjani huku na kule na nguvu alo nayo,timu pinzani humbeza kuwa hawezi kuwa mwanamke bali wanacheza na janadume,na ndipo sasa kituko kikaja kutokana na tuhuma hizo shirikisho la soka barani Africa walichagua njia ya kuhakiki jinsia ya Anonma.
Genoveva Anonma mwanasoka mwenye jinsi ya kike mwenye kasi ya ajabu michezoni aliamriwa kuvua nguo zake zote mbele ya maafisa wa CAF na mbele ya timu yake ya Equatoria Guine,nilifedheheka mno,hata ari ya mchezo ilishuka na nilikuwa nalia mno,ilikuwa ni udhalilishaji tosha,lakini ilinilazimu kutekeleza amri.
MAISHA YAKE.
Genoveva Anonma amekulia Equatorial Guinea na kadiri joto la kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika upande wa wanaume ikitarajiwa kuanza mwishoni mwa juma,tamaa yake ya kuwa msukuma gozi uwanjani inazidi kupanda,na tamaa hii haikuanza leo bali alipokuwa shuleni na hata nyumbani pia.

Anonma akiwajibika uwanjani
Anonma ameichezea Turbine Potsdam nchini Ujerumani katika ligi maarufu ya Bundesliga tangu mwaka 2011 .
Naye anasema,nilipokuwa na miaka mitano,huko kijijini kwetu wasichana walikuwa hawataki kucheza na mimi kwasababu nilikuwa napenda kucheza mpira wa miguu tu,hivyo muda mwingi nilikuwa nikicheza na wavulana tu anasema Anonma.
Baba yangu alikuwa anaishi katika mji mwingine na mwanamke mwingine, na mama yangu alikuwa akipambana name kila wakati niache kucheza mpira wa miguu,alikuwa akinitaka nisome hadi kufikia hatua ya digirii na niwe mwalimu ama nibobee katika masuala ya kuwasaidia watoto.
Tulikuwa hatuelewani,na akaapa kuwa hataki kuniona tena,name nikaondoka nyumbani na kwenda kuishi na mjomba wangu,mjombaangu hakuwa na matatizo nami akanipeleka mjini huko nikaendelea na masomo yangu na sikuacha kucheza mpira .
Anonma akapewa nafasi katika mji mkuu wa nchi yake Malabo alipokuwa na umri wa miaka 15 nazungumzia mwaka 2002.Hakuishia hapo mwaka mmoja baadaye alijiunga na timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,na baadaye akajiunga Jena ya Ujerumani ilikuwa katika ligi ya Bundesliga akiwa na timu hiyo aliwika na kuwa mfungaji bora wa Jena kwa misimu miwili mfululizo.
Mshindi wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka 2011 Nigeria, pamoja nan chi zingine ikiwemo Afrika Kusini,Ghana, waliishutumu Guinea kwakuwa na wachezaji watatu wa kiume katika timu yao wachezaji hao ni ndugu wawili Salimata na Bilguisa Simpore, na nahodha wao Anonma.
Taarifa za watatu hao kuwa ni wanaume zilipoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii Anonma akaamua kuvunja ukimya na kwenda mbele ya vyombo vya habari kukana shutuma hizo.
Na Anonma anadai kuwa yote hayo yanakuja kwasababu yey ni mwepesi na mwenye kasi ya ajabu awapo mchezoni,lakini najitambua kuwa mimi ni mwanamke.

CHANZO:BBC SWAHILI


No comments:

Post a Comment