RUAHA MEDIA
HABARI , MICHEZO , MATUKIO ,MAKALA , HABARI PICHA , BIASHARA , BURUDANI, VIPINDI VYA RADIO/TV
Sunday, 18 January 2015
Makanisa yachomwa Niger
Na; Calvin Stanley,Ruaha media
Maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed nchini Niger
Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao
Waandamanaji wachoma makanisa Niger
Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanawarushia mawe.
Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho cha utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.
Chanzo; bbcswahili
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment