Na: Calvin Stanley, Ruaha media
Katika miaka takribani 10 iliyopita
ulimwengu wa soka umetawaliwa na upinzani wa jadi kati ya wanasoka
wawili bora kabisa katika kizazi hiki, Mreno Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Lakini pamoja na upinzani walionao
uwanjani, wanasoka hao wawili wameonyesha kuwa na uhusiano mzuri
wanapokuwa nje ya uwanja, kwa pamoja wawili hao walionyesha hilo wakati
walipokuwa Uswisi mwanzoni mwa wiki hii kwenye sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d’Or.
Katika kuonyesha hawana uadui, Cristiano Ronaldo alisikika akimwambia Lionel Messi kwamba mwanae ambaye ni Cristiano JR ni shabiki wake mkubwa.
Alikaririwa akimwambia: “Mwanangu anakupenda sana, muda wote anaangalia video zako kwenye mtandao wa intaneti“– Cristiano Ronaldo.
CHANZO: millard ayo
No comments:
Post a Comment