RUAHA MEDIA
HABARI , MICHEZO , MATUKIO ,MAKALA , HABARI PICHA , BIASHARA , BURUDANI, VIPINDI VYA RADIO/TV
Sunday, 18 January 2015
Swansea yapokea kichapo.......
Na; Calvin Stanley,Ruaha Media
Diego Costa
Chelsea imeimarisha uongozi wake katika ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza kilabu ya Swansea mabao 5 bila jibu katika mechi iliodhibitiwa na chelsea kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar ndiye aliyefungua mtiririko huo wa mabao alipofunga sekunde chache tu baada ya mechi kuanza.
Mshambuliaji hatari wa Chelsea Diego Costa alifanya mambo kuwa magumu kwa Swansea baada ya kupachika bao la pili katika dakika ya 20 kabla ya kuongeza bao jengine katika dakika ya 34.
Fellaini
Oscar alifunga bao lake la pili na kuiweka Chelsea mbele na mabao 4-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili Swansea ilijitahidi na kuweza kukosa mabao ya wazi lakini ilipofikia dakika ya 79 Schurlle alifunga bao la tano.
Katika mechi nyingine Manchester United imeibuka mshindi kufuatia msururu wa matokeo mabaya baada ya kuichapa QPR mabao 2-0.
Marouane Fellaini na James Wilson walifunga mabao hayo yaliokuja katika kipindi cha pili katika uwanja wa Loftus Road.
liverpool
Nayo Liverpool iliendelea kumpa presha kocha wa Aston Villa Paul Lambert baada ya kuishinda Aston Villa na hivyo basi kupata ushindi wa tatu mfululizo.
Borini alifunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kabla ya lambert kumaliza kazi katika dakika ya 79.
Haya ndio matokeo ya mechi za jumamosi
Aston Villa 0 - 2 Liverpool
Burnley 2 - 3 Crystal Palace
Leicester 0 - 1 Stoke
QPR 0 - 2 Man Utd
Swansea 0 - 5 Chelsea
Tottenham 2 - 1 Sunderland
Chanzo; bbcswahili
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment