Wednesday, 14 January 2015

Hisa za Jiji katika Uda kujadiliwa bungeni

15th January 2015
Mabasi ya UDA.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imesema sakata la uhamishaji wa hisa za Jiji la Dar es Salaam kwenye kampuni ya UDA kwenda kwa Simon Group, litawasilishwa kwa Spika, ili kuangalia uwezekano wa kuliwasilisha bungeni kama hoja ya kamati na kujadiliwa na Wabunge.


Kadhalika, kamati umemtaka mjumbe wa kamati hiyo, Kangi Lugola, kuwasilisha nyaraka mbalimbali, ambazo kwa mujibu wa maelezo yake alisema hisa za Jiji zimeshahamishiwa kwa Simon Group na Meya wa Jiji na Mkurugenzi, wamesaini barua husika.


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajabu Mbarouk Mohamed, aliyasema hayo wakati kamati yake ilivyokutana na Meya wa Jijij, Dk. Didas Masaburi na Mkurugenzi wa Jiji, Wilison Kabwe, kujadili suala la Uda.


Awali, Lugola alisema alitumia siku ya jana kwenda kwa Msajili wa Makampuni (Brela) na kupata nyaraka mbalimbali zilizoonyesha Meya na Mkurugenzi wa Jiji, wakidai walisaini barua za kukubali kuhamishwa kwa hisa za Jiji kwenda kwa Simoni Group.
Baada ya kauli hiyo, Meya na Mkurugenzi huyo walitakiwa kuomba ardhi kama wamewadanganya wabunge, walisema iwapo itabainika ni kweli watajiuzlu nafasi zao.

Mjumbe Taulida Nyimbo, alimshutumu mwanasheria wa Jiji, Robert Mageni, kwa kuliingiza Jiji katika mkataba tata baina yao na Simoni Group, ambao unajichanganya kwa upande mmoja kusema ni wa miaka miwili na upande mwingine kuonesha ni mwaka mmoja.


Mwenyekiti alisema sehemu ya mkataba huo inamtaka Simon Group kulipa hisa zenye thamani ya Sh. bilioni 5.8 mara sita kwa miezi 24, lakini kuna kipengele kinataka alipe mara mbili ambayo ni sawa na mwaka mmoja.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment