RUAHA MEDIA
HABARI , MICHEZO , MATUKIO ,MAKALA , HABARI PICHA , BIASHARA , BURUDANI, VIPINDI VYA RADIO/TV
Wednesday, 14 January 2015
MAKALA YA UCHUMI ZISHINDE CHANGAMOTO UFANIKIWE KIMAISHA
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Maisha ya Mwanadamu yamejaa mitihani na majaribio ambayo ukifaulu unaingia kwenye ngazi nyingine ama kiwango kingine cha elimu,uchumi,mahusiano na kazi.
Wakati tukiwa tunasoma mashuleni ili kuingia darasa lingine ama kidato,mwaka mwingine wa masomo lazima upate mtihani ama majaribio ya kukupima kama unakidhi vigezo na viwango vya kuelekea katika hatua nyingine ya masomo.
Maisha tuliyonayo yana mitihani na majaribio ambayo tumezoea kuyaita Changamoto ,mbele ya changamoto kuna hatua nyingine zaidi ukiivuka changamoto ila usikubali kuishia hapo hapo kwasababu Mbele ya changamoto kuna kukua na kuongezeka.Nyuma ya changamoto kuna kudumaa,kudhoofu na kufa.
Katika safari ya kuyaelekea mafanikio kukutana na mafanikio ni lazima cha msingi usikate tamaa na kurudi nyuma jipe moyo songa mbele mpaka uyafikie mafanikio.
Vikwazo hivi vinafanana na virunzi mbele ya wanariadha wanaopiga mbio kuulekea ushindi ambayo ndio mafanikio.Unatakiwa kuviruka na kuulekea ushindi.Usibaki kwenye vizunzi sio mwisho uko ushindi mbele yako ruka upige mbio ufikie.
Katika Maisha wako walioruka virunzi na kufikia mafanikio/ushindi lakini pia wako waliobakia kwenye virunzi bila kusonga mbele na kubakia hapo wakilaumu virunzi,kuwalaumu wenzao,wazazi,walezi na serikali badala ya kuruka virunzi wayafikie mafanikio.
Hakuna mtu anaweza kuzuia mafanikio yako isipokuwa wewe mwenyewe.Maisha ni siri siri ya maisha yako unayo wewe na Muumba wako.
Amua kuruka virunzi,kusonga mbele,amua kushinda,kuzishinda changamoto zinazokukabili.Usiogope Utashinda.
Usiishi kwa kuziogopa changamoto jivike moyo wa ujasiri na kuamini kuwa umezaliwa ili ushinde na sio kushindwa.
Unaweza ukawa mshindi lakini si kwa mapambano yote ,weka nia ya kushinda ongeza bidii,ubunifu na nidhamu unaweza kuwa mshindi.
Utazikimbia changamoto mpaka lini wakati ndio mlango wa mafanikio,jitaidi uingie usitishwe na ukubwa wa mlango kwani “UKUMBWA WA MAFANIKIO NDIO UKUMBWA WA MAFANIKIO YALIYOKO MBELE YAKO”.
Changamoto si adui ni rafiki anayetaka kukupeleka kwenye hatua nyingine ya ubunifu,maboresho na mafanikio .
Changamoto zinakutaka ukatae kuishi kwa mazoea,kufanya kazi kwa mazoea,kufanya biashara kwa mazoea,kuongoza kwa mazoea,kubadilika kulingana na wakati na mahitaji ya watu.kwasababu dunia tunayoishi ina kila aina ya ushindani.
Watu wasiotaka kubadilika wanazichukia changamoto kuzipiga vita badala ya kuzielewa na kukabiliana nazo na kuzishinda hivyo wanajikuta wakigonga ukuta ama kuangukia pua.
Kwenye maisha hakuna kitu rahisi hivyo bidii na nidhamu ni kitu muhimu sana katika maisha ya mtu yoyote anayehitaji mafanikio iwe katika uchumi,elimu,mahusiano,siasa.
Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani lazima ndoto hiyo ipite kwenye barabara ya changarawe,miba,mawe ,mabonde ambazo ndio changamoto ili ziweze kufanikiwa.
Hakuna ndoto iliyowahi kupita redcarpet ndoto nyingi zimepitia magumu mpaka zikafanikiwa,hivyo ukiwa na ndoto usitegemee kupigiwa makofi.Hata dhahabu hujaribiwa kwa kupitishwa kwenye moto ili iwe safi na yenye thamani kubwa.
ferdinandshayo@gmail.com
0765938008
CHANZO. PRINCEMEDIATZ
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment