Serikali
ya Ufaransa imewataka waendesha mashtaka kuchukua hatua thabiti dhidi
ya Watu waliotekeleza vitendo vya kigaidi.Waziri wa Sheria nchini
humo,Christiane Taubira amesema maneno au vitendo vya chuki dhidi ya
mwingine vinavyotolewa kwa sababu ya imani ya dini vikomeshwe
.
Zaidi
ya Kesi 50 zimefunguliwa dhidi ya Watu wanaotuhumiwa kuhusikana
shambulio la kigaidi wiki iliyopita na kusababisha watu 17 kupoteza
maisha.Miongoni mwa walio matatani ni Said Koachi sambamba na
shemejiye.Wakili wa Said ameiambia BBC kuwa Said alikuwa katika hali ya
kawaida kabla ya shambulio kutokea.Wakati hayo yakijiri,kumekuwa na mapokeo hasi kwa Waumini wa kiislamu baada ya kuchapishwa kwa Jarida lenye kibonzo kinachomuonyesha Mtume Mohamad akiomboleza.
Kiongozi mmoja wa kidini na Mufti wa Jerusalem ameita chapisho huwa kuwa ni tusi.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Jordan,Nasser Joudeh amesema Charlie Hebdo kwa mara nyingine inapandikiza mbegu za chuki na migogoro.
Nako mjini Nouakchott, Polisi wamezuia maandamano ya Watu waliokuwa wakielekea Ubalozi wa Ufaransa, huku Mahakama ya Uturuki nayo ikipiga marufku kuchapishwa kwa Gazeti la Charlie Hebdo lenye kibonzo hicho
CHANZO : BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment