Habari na Rehema Mbowe.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha [AJTC] wamejumuika kwa pamoja kufanya usafi katika soko la
mbauda jijini Arusha.
Zoezi hilo
lilifanyika mapema jana na wanafunzi katika ngazi ya stashahada [Ruaha na Tarangire]
ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao pia kutimiza wajibu wao katika jamii.
Aidha mmoja
wa wanafunzi hao kutoka darasa la Tarangire Sinyata Kilusu amesema wao ni ni
waandiashi wa habari hivyo wanapaswa kua mfano mzuri kwa jamii kwa kufanya
shughuli mbali mbali za kijamii.
“Sisi
waandishi wa habari ni vioo vya jamii hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano na
mchango wetu wa hali na mali kwenye mambo mbali mbali katika jamii” akisema
Sinyati.
Hata hivyo
afisa afya wa kata ya Sombetini Bi Beatha Gitagno alihitimisha kwa kutoa
shukrani za dhati kwa wanafunzi na uongozi wa AJTC kwa umoja na ushirikiano wao
katika kufanya usafi sokoni hapo.
No comments:
Post a Comment