Wednesday, 11 February 2015

WANAFUNZI WA AJTC WAFANYA USAFI SOKO LA MBAUDA JIJINI ARUSHA

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha{PICHA NA Maria Thobias}




Habari na Maria Thobias
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha AJTC  wamefanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha.


Wanafunzi hao wa ngazi ya stashahada katika madarasa ya Ruaha na Tarangire wamefanya usafi  katika soko hilo mapema jana ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.


Mmoja kati ya wanafunzi hao anayefahamika kwa jina la Agnes Kinisa amesema kuwa zoezi hilo litajenga na kuendeleza mahusiano mazuri kati yao na jamii pia kuwajenga katika misingi bora ya kufanya kazi kwa ufanisi watakapokua makazini.


“Kwa kufanya usafi hapa sokoni tutajenga na kuendeleza mahusiano mazuri kati yetu sisi wanafunzi, chuo kwa ujumla, jamii ikizingatia tunasoma tuende makazini hili litatuongezea ufanisi zaidi kazini”Alisema Agnes.


Aidha afisa afya wa kata ya Sombetini Bi Beatha Gitagno amewashukuru sana wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono tena na kusema watawaelimisha walioko nyuma yao.


Soko hilo hilo linolohudumia wakazi wengi wa ndani na nje ya jiji la Arusha linahitaji marekebisho makubwa ikiwemo kijengewa uzio pampja na kuongezwa wafanyakazi wa kusafiha soko hilo kwani waliopo hawamudu kulingana na uchache wao.

No comments:

Post a Comment