Wednesday, 11 February 2015

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA WAWASHUKURU CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA


Na Elizabeth Betha , ruaha medi
Arusha

Wakazi wa Mbauda  wamekipongeza chuo  Cha Uandishi  wa habari na Utangazaji Arusha kwa  kujitolea kufanya usafi katika soko la mbauda  kama mchango wao kwa jamii.

Akizungumza na wanafunzi hao pamoja na  waandishi wa habari waliofika sokoni hapo  Afisa afya wa kata ya Sombetini Beatha Gitaguo alisema kuwa wamefurahishwa na jambo hilo  kwani ni ushirikiano mzuri kati ya chuo na jamii inayowazunguka na kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwaelimisha  walioko nyuma yao .

“Tumeshukuru sana kwa ujio wenu wakuamua  kutuunga mkono katika swala la usafi na hivi mlivyofanya hata wanajamii wamejiuliza maswali   kama nyinyi msiyohusika na soko hili mmeamua kufanya usafi je wao si zaidi katika kufanya hivyo” alihoji  Beatha  

Hata hivyo alisema kuwa katika soko hilo linakabiliwa na  uhaba wa wafanyakazi wa kufagia  ambapo alisema wapo watatu kwa eneo lote na kuongeza kuwa miundo mbinu ya soko hilo haijakaa sawa hivyo huwapa wafagiaji tabu wakati wakufagia.
 
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha  wakiendele na usafi sokoni hapo (Picha na Elizabeth Betha, Ruaha Media )

Naye  mkufunzi wa chuo hicho Verediana  Akonaye alisema lengo lao kufanya hivyo ni ili kujenga mahusiano mazuri na jamii na kama waandishi wa habari na maafisa uhusiano watarajiwa  ni lazima kuchangamana katika shughuli za kijamii.

Aliongeza kuwa  chuo hicho pia kinaandaa  maafisa mahusiano   hivyo  kazi za kijamii ni moja ya aina za kampeni ya  kuhamasisha kampeni  za kampuni flani.

Kwa upande wake  mmoja wa wafanya biashara wa soko hilo Hassani  Athumani alisema kuwa wao kama wafanya biashara wamefurahishwa na jambo hilo kwa kuwa usafi ni nyenzo muhimu kwa maisha ya binadamu   ambapo  aliongeza kuwa kutokana na uchache wa wafagiaji wa soko hilo wamekuwa wakizidiwa na wakati mwingine kushindwa kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment