Wednesday, 11 February 2015

WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WAFAGIA SOKO LA MBAUDA JIJINI ARUSHA

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha.{PICHA NA Digna Mushi}




Habari na Digna Mushi

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wamejitolea kufanya usafi katika soko la Mbauda lililopo jijini Arusha.
        
Wanafunzi hao wanaosomea kozi ya uandishi wa habari na utangazaji ngazi ya stashahada wanaotokea madarasa ya Ruaha na Tarangire wameamua kufanya hivyo ikiwa ni moja kati ya majukumu yao kama vioo vya jamii.

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina Maria Thobias Kavishe amesema kua wao ni vioo vya jamii hivyo ni jukumu lao kushiriki katika kazi za kijamii.

“Sisi kama waandishi wa habari tuna majukumu mengi ikiwa ni kuihamasisha na kuielimisha jamii mambo mbali mbali wasiyoyajua . Hivyo kufanya usafi ni mojawapo ya njia ya kuielimisha na kuihamasisha jamii yetu” alisema mwanafunzi huyo.

Aidha afisa afya wa kata ya Sombetini Bi Betha Gitago amewashuru  wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono kwa kua wameihamasisha na kuilimisha jamii kwa namna moja au nyingine.

Pia aliogeza kwa kuwasihi na kuwaomba  wanafunzi hao kua wawe na moyo huo huo walionao hata baada ya kumaliza mafunzo yao kwani jamii inawategemea katika kuwaelimisha

No comments:

Post a Comment