Mmoja wa wanafunzi katika chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha Lidya Kishia (pichani) akifanya usafi katika soko la Mbauda.Picha na Martin Masawe.
Wanafunzi wa
chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha wamejitolea kufanya
usafi katika soko la mbauda kama mojawapo ya shughuli za kijamii ili kuonyesha mfano kwa jamii ikiwa wao ni
kioo cha jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkufunzi wa chuo
hicho Verediana Akonaye, alisema lengo
lao kufanya hivyo ni ili kujenga mahusiano mazuri na jamii kama waandishi wa habari na maafisa uhusiano
watarajiwa, katika kuchangamana na
shughuli za kijamii.
Naye afisa afya
wa kata ya Sombetini ndugu Beatha Gitaguo amesema kuwa wamefurahishwa na jambo
hilo kwani ni ushirikiano mzuri kati ya
chuo na jamii inayowazunguka kwani kwa kufanya hivyo ni kuielimisha jamii
kuhusu umuhimu wa kuyaweka mazingira yanayowazunguka katika hali ya usafi.
“Tumeshukuru
sana kwa ujio wenu wa kuamua kutuunga
mkono katika suala la usafi, na hivi mlivyofanya hata wanajamii wamejiuliza
maswali mengi kama nyinyi msiohusika na soko hili mmeamua kufanya usafi je wao
si zaidi katika kufanya hivyo?”alisema Beatha.
Pamoja na hayo alisema kuwa soko hilo lina
wafanyakazi watatu wa kufagia katika eneo lote la soko, na hivyo kuwapa tabu
wakati wa kufagia kutokana na
miundombinu ya soko hilo kuwa mibovu.
Kwa upande wake mmoja wa wafanya biashara wa soko hilo
Hassani Athumani alisema kuwa
amefurahishwa na jambo hilo na kusema
kuwa usafi ni nyenzo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Kutokana na kufanyika kwa usafi eneo hilo wakazi watumiaji wa soko
la mbauda, wamewapongeza wanafunzi wa
chuo hicho kwa kujitolea kufanya usafi katika soko hilo na
kuwataka wawahamasishe jamii kuzingatia usafi ili waweze kuepukana na maradhi.
No comments:
Post a Comment