HABARI , MICHEZO , MATUKIO ,MAKALA , HABARI PICHA , BIASHARA , BURUDANI, VIPINDI VYA RADIO/TV
Wednesday, 4 March 2015
HABARI PICHA Ziara katika hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara
Na Tumaini Mafie , Ruaha Media |
Katikati ni makamu mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Elifuraha Samboto akiwa na wanafunzi wa darasa la Ruaha katika chuo hicho walipotembelea hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara (Picha na Tumaini Mafie , Ruaha Media ) |
TAZAMA HAPA PICHA ZA WANYAMAPORI KATIKA HIFADHI YA ZIWA MANYARA.
Twiga akila majani katika hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara(picha na DIGNA MUSHI Ruaha media)
Tembo katika hifadhi ya taifa ya ziwa manyara (picha na DIGNA MUSHA, Ruaha media)
HABARI PICHA : Tazama wanyama wanaopatikana ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Manyara
UTALII KATIKA HIFADHI YA MANYARA
Wanafunzi wa Arusha Journalism walipotembelea Ziwa Manyara mwishoni mwa wiki.(Picha na;Evaline Mollel)
Mnyama aina ya Tembo anaepatikana katika hifadhi ya Manyara.(Picha na; Evaline Mollel)
Tuesday, 3 March 2015
KIVUTIO CHA HIFADHI YA MANYARA
Na Martin Masawe/Ruaha Media
Mnyama mrefu kuliko wote katika hifadhi ya ziwa Manyara Twiga,akijitafutia chakula kwenye miti iliyopo kwenye hifadhi hiyo.(picha na Martin Masawe)
Mnyama mrefu kuliko wote katika hifadhi ya ziwa Manyara Twiga,akijitafutia chakula kwenye miti iliyopo kwenye hifadhi hiyo.(picha na Martin Masawe)
Wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika usafiri wa baiskeli kuelekea kuliona ziwa manyara (mbeleni) katika moja ya safari za kimasomo.(picha na martin masawe)
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari watembelea hifadhi ya ziwa manyara
na Agness Kinisa, Ruaha Media
twiga wanopatikana katika hifadhi ya manyara. (picha na Agness Kinisa)HABARI PICHA : Wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha watembelea Hifadhi ya Taifa Ya Manyara
ijue hifadhi ya manyara
na Diana Ringo, Ruaha Media.
wanyama aina ya nyati wanao patikana katika hifadhi ya ziwa manyara. (picha na Diana Ringo).
maji moto yanayopatokana katika hifadhi ya ziwa manyara. (picha na Diana Ringo).
ziara ya kimasomo ndani ya hifadhi ya ziwa manyara
na Esther Danford, Ruaha Media.
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji wakiwa katika picha ya pamoja ufukweni mwa ziwa manyara. (picha na Esther Danford).
UTALII MARIDHAWA
Na; Elizabeth Betha(Ruaha Media)
Pichani mnyama Twiga ambaye ni kivutio katika Hifadhi ya Ziwa Manyara.(Picha na Elizabeth Betha)
Pichani mkufunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha akishiriki zoezi la kuendesha baiskeli kutembelea vijiji vinavyopatikana katika mji wa Mto wa Mbu.(Picha na Elizabeth Betha)
UTALII WA NDANI
Na;Calvin Stanley
Wanafunzi wa darasa la Ruaha kutoka chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye ziara yao katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.(Picha na;Calvin Stanley)
Pichani wanyama aina ya Tembo ambao ni moja kati ya vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.(Picha na Calvin Stanley)
Saturday, 21 February 2015
Wednesday, 11 February 2015
USAFI NI AFYA
Na;Martin Masawe,Ruaha Media
Mmoja wa wanafunzi katika chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha Lidya Kishia (pichani) akifanya usafi katika soko la Mbauda.Picha na Martin Masawe.
Mmoja wa wanafunzi katika chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha Lidya Kishia (pichani) akifanya usafi katika soko la Mbauda.Picha na Martin Masawe.
Wanafunzi wa
chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha wamejitolea kufanya
usafi katika soko la mbauda kama mojawapo ya shughuli za kijamii ili kuonyesha mfano kwa jamii ikiwa wao ni
kioo cha jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkufunzi wa chuo
hicho Verediana Akonaye, alisema lengo
lao kufanya hivyo ni ili kujenga mahusiano mazuri na jamii kama waandishi wa habari na maafisa uhusiano
watarajiwa, katika kuchangamana na
shughuli za kijamii.
Naye afisa afya
wa kata ya Sombetini ndugu Beatha Gitaguo amesema kuwa wamefurahishwa na jambo
hilo kwani ni ushirikiano mzuri kati ya
chuo na jamii inayowazunguka kwani kwa kufanya hivyo ni kuielimisha jamii
kuhusu umuhimu wa kuyaweka mazingira yanayowazunguka katika hali ya usafi.
“Tumeshukuru
sana kwa ujio wenu wa kuamua kutuunga
mkono katika suala la usafi, na hivi mlivyofanya hata wanajamii wamejiuliza
maswali mengi kama nyinyi msiohusika na soko hili mmeamua kufanya usafi je wao
si zaidi katika kufanya hivyo?”alisema Beatha.
Pamoja na hayo alisema kuwa soko hilo lina
wafanyakazi watatu wa kufagia katika eneo lote la soko, na hivyo kuwapa tabu
wakati wa kufagia kutokana na
miundombinu ya soko hilo kuwa mibovu.
Kwa upande wake mmoja wa wafanya biashara wa soko hilo
Hassani Athumani alisema kuwa
amefurahishwa na jambo hilo na kusema
kuwa usafi ni nyenzo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Kutokana na kufanyika kwa usafi eneo hilo wakazi watumiaji wa soko
la mbauda, wamewapongeza wanafunzi wa
chuo hicho kwa kujitolea kufanya usafi katika soko hilo na
kuwataka wawahamasishe jamii kuzingatia usafi ili waweze kuepukana na maradhi.
CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA CHAPONGEZWA
Na Tumaini
Mafie
Arusha
Wakazi wa Mbauda wamekipongeza chuo Cha Uandishi
wa habari na Utangazaji Arusha kwa
kujitolea kufanya usafi katika soko la mbauda kama mchango wao kwa jamii.
Akizungumza
na wanafunzi hao pamoja na waandishi wa
habari waliofika sokoni hapo Afisa afya
wa kata ya Sombetini Beatha Gitaguo alisema kuwa wamefurahishwa na jambo
hilo kwani ni ushirikiano mzuri kati ya
chuo na jamii inayowazunguka na kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwaelimisha walioko nyuma yao .
“Tumeshukuru
sana kwa ujio wenu wakuamua kutuunga
mkono katika swala la usafi na hivi mlivyofanya hata wanajamii wamejiuliza
maswali kama nyinyi msiyohusika na soko
hili mmeamua kufanya usafi je wao si zaidi katika kufanya hivyo” alihoji Beatha
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa ha bari na utangazaji Arusha wakiwa na mkufunzi waa chuo hicho wakizoa takataka katika soko la Mbauda (Picha na Tumaini Mafie , ruaha media) |
Hata hivyo
alisema kuwa katika soko hilo linakabiliwa na
uhaba wa wafanyakazi wa kufagia
ambapo alisema wapo watatu kwa eneo lote na kuongeza kuwa miundo mbinu
ya soko hilo haijakaa sawa hivyo huwapa wafagiaji tabu wakati wakufagia.
Naye mkufunzi wa chuo hicho Verediana Akonaye alisema lengo lao kufanya hivyo ni
ili kujenga mahusiano mazuri na jamii na kama waandishi wa habari na maafisa
uhusiano watarajiwa ni lazima
kuchangamana katika shughuli za kijamii.
Aliongeza
kuwa chuo hicho pia kinaandaa maafisa mahusiano hivyo
kazi za kijamii ni moja ya aina za kampeni ya kuhamasisha kampeni za kampuni flani.
Kwa upande
wake mmoja wa wafanya biashara wa soko
hilo Hassani Athumani alisema kuwa wao
kama wafanya biashara wamefurahishwa na jambo hilo kwa kuwa usafi ni nyenzo
muhimu kwa maisha ya binadamu ambapo aliongeza
kuwa kutokana na uchache wa wafagiaji wa soko hilo wamekuwa wakizidiwa na
wakati mwingine kushindwa kufanya vizuri.
MWISHO.
WAUNGWANA HUWA NI WASAFI
Na Evalline Mollel
Arusha
Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha. Picha na EVALINE MOLLEL
Mwenyekiti
wa kata ya Sombetini bw.Prosper mollel ametoa shukrani kwa wanafunzi wa chuo
cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kwa kufanya usafi katika soko la
Mbauda jijini Arusha.
Ametoa
shukrani hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na wanafunzi hao mara baada ya
zoezi hilo kumalizika ambapo amesema kuwa wamesaidia sana katika kuweka mazingira ya soko hilo kuwa saf.i
Naye bi.
Afya wa kata hiyo Beatha Gitaguo amewashukuru wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono
katika suala la usafi na kusema kuwa itakuwa fundisho kwa wanafunzi na watu
wengine kufanya kitendo kama hicho katika maeneo mbalimbali yanayowazunguka.
Amesema soko
hilo limekuwa chafu kwa muda mrefu licha ya kuwa wawakilishi kutoka halmashauri
ya jiji wamekuwa wakilisafisha lakini bado hali ya uchafu inaongezeka kutokana
na wawakilishi hao kuwa wachache na kukosa
ushirikiano kutoka kwa wananchi.
Kwa upande
wa wanafunzi hao wamesema suala la kujitoa kufanya shughuli za kijamii kama
kufanya usafi sehemu mbalimbali,kutembelea vituo vya watoto yatima hata
wagonjwa,ni wajibu wa kila mtu na siyo wahusika pekee.
Wamesema
lengo lao la kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha uhusiano baina yao na jamii
inayowazunguka kwani wao ni sehemu ya jamii na jamii ni wao hivyo ni jukumu lao
kufanya hivyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)